1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mahakama ya ICC kusikiliza rufaa ya Dominic Ongwen

Josephat Charo
14 Februari 2022

Mahamakama ya kimataifa inayoshughulikia kesi za uhalifu wa kivita, ICC ,inatarajiwa kuanza kusikiliza rufaa ya Dominic Ongwen Jumatatu.

https://p.dw.com/p/46ysB
Den Haag | ICC verurteilt Warlord Dominic Ongwen aus Uganda
Picha: ICC/AA/picture alliance

Kamanda wa zamani wa kundi la waasi la Lord's Resistance Army, LRA. Ongwen amekata rufaa kutiwa hatiani kwa makosa ya uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu.

Ongwen, ambaye zamani alilitumikia kundi hilo linaloongozwa na Joseph Kony kama mwanajeshi alipokuwa mtoto mdogo, alihukumiwa na mahakma ya ICC mnamo Mei mwaka uliopita kifungo cha miaka 25 baada ya kutiwa hatiani kwa mauaji, ubakaji na utumwa wa ngono.

Katika taarifa yake, mahakama ya ICC imesema rufaa iliyowasilishwa ndiyo kubwa kabisa kuwahi kuzingatiwa huku ikiibua masuala mazito na muhimu.

Mahakama hiyo imeseama rufaa hio itasikilizwa kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa.