1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Serikali ya UK yakwaa kisiki uhamishaji waomba hifadhi

Josephat Charo
29 Juni 2023

Mahakama ya rufaa jijini London imeamua leo kwamba mpango wa Uingereza kuwapeleka Rwanda wakimbizi wanaoomba hifadhi si halali kisheria.

https://p.dw.com/p/4TDJD
Großbritannien Proteste gegen die Abschiebung nach Ruanda
Picha: Niklas Hallen/AFP/Getty Images

Mjaji wa mahaka hiyo wamesema Rwanda haiwezi kuzingatiwa kama ya tatu iliyo salama ambako wakimbizi wanaweza kupelekwa. Serikali ya Uingereza inatarajiwa kuakta rufaa hukumu hiyo katika mahakama ya juu kabisa ya nchi hiyo.

Hukumu hiyo huenda ikaamua mustakhbali wa ahadi ya waziri mkuu wa Uingereza Rishi Sunak kuzuia wahamiaji kuwasili nchini huko kwa njia ya boti.

Kwa mujibu wa mkataba ulioafikiwa mwaka uliopita, serikali ya Uingereza inapanga kuwasafirisha hadi nchini Rwanda maalfu kwa maalfu ya wakimbizi wanaowasili katika fukwe zake zaidi ya kilometa 6,400 katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki.

Safari ya kwanza ya ndege ya kuwapeleka wakimbizi Rwanda ilizuiwa mwaka mmoja uliopita katika uamuzi wa dakika ya mwisho uliopitishwa na mahakama ya Ulaya ya Haki za binadamu, iliyoweka zuio mpaka mchakato wa kisheria utakapokamilika Uingereza.