Ujerumani: Chama cha siasa kali chanyimwa ruzuku ya serikali
23 Januari 2024Matangazo
Uamuzi huo ulitolewa na Mahakama ya Katiba ya Ujerumani hii leo baada ya mchakato mrefu. Chama hicho cha Die Heimat pia kitaondolewa upendeleo wa kodi inayotolewa kwa vyama na michango ya kisiasa.
Mwaka 2017 mahakama hiyo ya katiba iliamua kuwa chama hicho, wakati huo kikiwa NPD kilikuwa kinayumbisha utaratibu wa kikatiba na kidemokrasia nchini Ujerumani. Lakini mahakama hiyo haikukifungia chama hicho ikisema hakiungwi mkono na wengi na hakitoi kitisho kikubwa.
Soma pia: Korti ya katiba yasema chama cha NPD hakina madhara
Hata hivyo, bunge la Ujerumani lilijibu kauli hiyo kwa kupitisha sheria mpya inayoruhusu vyama vilivyo na siasa kali kutofadhiliwa na serikali na kuondolewa upendeleo wa kodi.