UchumiUlaya
Mahakama kuu ya Ulaya yaamuru Google na Apple kulipa kodi
10 Septemba 2024Matangazo
Kesi hizo mbili zilikuwa sehemu ya mapambano ya Umoja wa Ulaya kukomesha mianya ya kodi na udhibiti wa makampuni makubwa ya teknolojia ya Marekani.
Mahakama ya Haki ya Ulaya ECJ imeunga mkono hukumu iliyotolewa mwaka 2016 na Tume ya Ulaya kwamba Apple inapaswa kulipa kodi ya euro bilioni 13 na kubatilisha uamuzi wa awali uliokuwa upande wa Apple.
Tume ya Ulaya ilisema katika hukumu ya mwaka 2016, kuwa kampuni ya Apple ililipa kodi kidogo kufuatia makubaliano yasiyo halali na mwanachama wa Umoja wa Ulaya Ireland.