Mahakama Kuu ya Kenya imetoa uamuzi wa kutouzuia mchakato unaosubiriwa kwa hamu wa kumuondoa madarakani Naibu wa Rais Rigathi Gachagua. Uamuzi huo wa Jumatatu umekuja katika wakati ambapo kiongozi huyo anayetofautiana na mkuu wake, Rais William Ruto akiomuomba radhi rais na wanachi wa Kenya. Saumu Mwasimba alizungumza na mkuu wa baraza la waandishi habari wa kimataifa Kennedy Wandera.