1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Magazetini: Ziara ya Macron Marekani

Sekione Kitojo
26 Aprili 2018

Wahariri wa magazeti ya Ujerumani wamezungumzia zaidi kuhusu ziara ya rais wa Ufaransa Emmanuel Macron nchini Marekani,ongezeko la chuki dhidi ya wayahudi nchini Ujerumani, na pia kuhusiana na ais mpya wa Cuba.

https://p.dw.com/p/2wiMB
USA Washington - Donald Trump trifft Emmanuel Macron - Gala
Picha: Getty Images/C. Kleponis

 

Tukianza  na  gazeti  la  Badische Zeitung  la  mjini Freiburg  kuhusu  ziara  ya  Macron  nchini  Marekani, mhariri wake anaandika:

"Emmanuel Macron amekabiliana  na  karibu  kila  kitu ambacho  kiongozi  anachoweza  kukabiliana  nacho  katika ziara  ya  kitaifa  alipokutana na  Donald Trump. Kushikana mikono kwa  nguvu, mkono  katika  bega kila wakati, busu nyingi  ambazo  mtu  hajawahi  kuziona  katika  Ikulu  ya Marekani  ya  White House. Macron anaingia  katika  hatari kubwa anasema mhariri. Wakati  Macron anayefuata  sera za  kimataifa  na  Trump  anayefuata  zera  za  kizalendo zaidi  wakijiweka  pamoja, akitaka, mbali  ya  kwamba wanatofautiana  kuhusiana  na  mkataba  wa  Iran, lakini anataka  kujenga uhusiano  imara  na  Trump. Ni  katika mtazamo  huu  tu  ambapo kila  uhusiano  wa  kisiasa  ni suala ambalo linaweza kufanyiwa majadiliano iwapo  kuna maslahi. Macron, mhariri  anaadika  anaweza  hatimaye kuondoka  mikono  mitupu."

Kuhusu ziara  hiyo ya  Macron  nchini  Marekani, mhariri wa  gazeti  la  Mannheimer Morgen anasema  baada  ya ziara hiyo iliyokuwa  na  mapenzi  makubwa  ya  Emmanuel Macron  mjini  Washington, Donald Trump  anatarajia kukutana  na  Angela  Merkel  kesho  katika  ziara  ambayo ni  tofauti  kabisa na  yenye majadiliano  magumu. Mhariri anaadika:

"Majukumu  yanaonekana  kuwa yamsingi  kabisa. Rais  wa Ufaransa  alitayarisha  uwanja kwa  hisia,  kansela  wa Ujerumani  yeye  atakuwa  anajadili  kwa njia ya ukakamavu zaidi. Timu  ya  Ulaya  ya  M na M, Macron  na  Merkel inalenga  katika  lengo  moja. Linahusu  kuokoa makubaliano  ya  kinyuklia  na  Iran pamoja  na  kuzuwia ongezeko  la  ushuru  wa  forodha kwa  bidhaa  za  chuma na  bati  kutoka  katika  mataifa  ya  Umoja  wa  Ulaya."

Chuki dhidi ya wayahudi

Tunavaa  Kippa.  Anaandika  mhariri  wa  gazeti  la  Rhein-Neckar-Zeitung  la  mjini  Heidelberg  kuhusiana  na  vikofia wanavyovaa  Wayahudi  kuhusiana  na  mada  ya kuongezeka  kwa  chuki  dhidi  ya  Wayahudi  nchini Ujerumani. Mhariri  anaandika:

"Tulipaswa  kuonesha  wazi  kwamba  tunavaa  vikofia  hivyo na  huenda ilitakiwa  kufanya  hivyo  mapema  zaidi, ili kuzuwia  hali  ya  kutoeleweka. Kwamba  Ujerumani inaikosoa  Israel , kama  yalivyo  mataifa  mengine, ni sahihi  na  ni  haki kabisa. Lakini  ukosoaji  huo  hata  hivyo si  suala  la  kuikana kabisa  Israel, badala  yake  ni  katika hali  hiyo  tu,  ambayo  ni  katika  kutofautiana   kimawazo. Tunavaa Kippa, tunavaa  hijabu. Na  kwa  kiasi  kikubwa tunavaa  misalaba. Haya  yote  yanapatikana  nchini Ujerumani. Kwa  hakika  ni  ujumbe  wa  wazi  wa kuvumiliana."

Nae mhariri  wa  gazeti  la  Hannoversche Allgemeine Zeitung  akizungumzia  mada  hiyo  anaandika:

"Mshikamano  dhidi  ya  chuki  kwa  Wayahudi  ni  ujumbe muhimu kwa  sasa. Mjadala  kuhusu  chuki  dhidi  ya Wayahudi  katika  nyimbo za  kurap nchini  Ujerumani, vidio za  kushitua  za   mashambulizi dhidi  ya  kijana  wa Kiisraeli  aliyevaa  kibandiko mjini  Berlin, maadhimisho  ya miaka  70 ya  kuundwa  kwa  taifa  la  Israel, haya  yote yalikuja  kwa  pamoja  wiki  iliyopita na  ilikuwa  ni  ajenda ya  kisiasa. Lakini  kama  kawaida, pamoja  na  hayo  yote, kuna kitisho cha  kuporomoka  kwa  ishara  ya mshikamano,  na   kupotea  kwa  maadili. Mtu hapambani dhidi  ya  chuki  dhidi  ya  Wayahudi  jioni. Na  hii  sio katika  fikira  za  wanazi mamboleo  ama  Waislamu  wenye itikadi  kali pekee,  lakini  hata  katika  hukumu  na kupunguza nadharia ambazo  hazijafanyiwa  uchunguzi."

Kuhusu mada ya mwisho ya  rais  mpya  wa  Cuba, gazeti la  Rheinpfalz  la   mjini  Ludwigshafen linaandika:

"Kwanza  kabisa  hilo  sio  jambo  jipya  mjini  Havanna. Jumuiya  ya  kimataifa  na  hususan  Wacuba  wenyewe watalazimika  kuwa  wavumilivu, wakati  rais  wao  mpya anafahamu  matatizo  na  mahitaji  ya  kizazi  cha  vijana , na  kujishughulisha  nayo  kuliko  marais   waliopita. Pamoja  na  hayo  mageuzi  yatakuwa  machache na ya juu juu  tu  kama  yatafanyika. Hayatatosha , kuweza  kuzuwia kuporomoka."

Hayo  ndio kwa  muhtasari  maoni  ya  wahariri wa magazeti ya  Ujerumani   kama  yalivyokusanywa  na  Sekione Kitojo.

Mwandishi: Sekione  Kitojo / Inlandspresse

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman