Magazetini: Vita nchini Syria, SPD, Macron na wakimbizi
22 Februari 2018Tukianza na mada inayozungumzia vita nchini Syria, gazeti la Tagesspiegel la mjini Berlin linazungumzia kuhusu mkataba wa Geneva kuhusu vita:
Mkataba wa Geneva unayataka mataifa yote duniani kuwalinda raia. Ni marufuku kushambulia hospitali, kuwazingira raia na kuwaweka katika hali ya kutopata chakula kama silaha ya kivita ni marufuku , na pia ni lazima kulinda misafara ya mashirika ya kutoa misaada. Nchini Syria mhariri anaandika mambo haya tuliyojiwekea hayana maana tena, hata kwa suala la matumizi ya silaha za sumu. Vita nchini Syria imeingia katika hali ya unyama mkubwa, ni kutokana na kejeli pamoja na udhaifu wa nchi zenye dhamana za kuwalinda watu nchini Syria kama Urusi na Iran. Pia ni kutokana na Marekani kuonekana kuchoka. Uturuki pia ina mchango wake katika hili, kwa kujitoa kutoka katika maadili ya NATO. Na mataifa mengine ya NATO yanatazama tu.
Mhariri wa gazeti la Stuttgarter Zeitung anazungumzia kuhusu vita ya dunia katika mfumo wa kanda:
Hali inayosikitisha nchini Syria ni kwamba kwa muda mrefu sasa hakuna tena nchi yenye nguvu na mamlaka, ambayo inaweza kuzuwia mauaji ya holela nchini humo. Nchini Syria hivi sasa kunatokea vita ya dunia katika mfumo wa kikanda, kila mmoja anashiriki katika mzozo huo na amechukua jukumu la kuwa mpatanishi.
Wanachama wa SPD
Wanachama wa chama cha Social Democratic SPD wanapiga kura kuamua iwapo chama chao kishiriki katika serikali ya muungano na wahafidhina wanaoongozwa na kansela Angela Merkel ama la. Mhariri wa gazeti la Münchner Merkur anatoa picha ya chama hicho:
Chama cha SPD kimo katika manung'uniko, na baadhi ya vyombo vya habari vinaitumia hali hiyo. Hata kama viongozi wa juu wa chama hicho , wamefanya makosa makubwa , inatarajiwa takriban kuweka heshima kidogo pamoja na haki. Hii ni kutokana na haki ya wanachama 460,000 , ambao katika siku za hivi karibuni sio tu watapiga kura kuidhinisha muungano wa kuunda serikali, lakini pia mustakabali wa chama hicho. Wanafanya hivyo kwa kujitambua na hata kama vyama vikuu vya Ujerumani vikiwa katika hali ya matatizo.
Kuhusu sera za rais wa Ufaransa kwa wakimbizi, gazeti la Fuldaer Zeitung linaandika:
Katika sera kuhusu wakimbizi mahakama ya Ulaya iko wazi, na kwamba hali inajirudia tena. Mapambano ya kulinda mifumo ya utamaduni, dini na siasa, vitu ambavyo wakimbizi kutoka Afrika kaskazini wanaonekana kuwa wamepitia katika hali ya kutisha sana, wanapaswa kujishauri iwapo wanahitajika kuja katika nchi kama za Ulaya.
Mwandishi: Sekione Kitojo/Inlandspresse
Mhariri: Josephat Charo