1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mafuriko yasababisha uharibifu Ujerumani

13 Julai 2024

Maafa makubwa zaidi yameshuhudiwa katika miji ya jimbo la Bavaria na maeneo ya mpakani na Austria ambako barabara nyingi zimefunikwa na maji, miti ikianguka na kupelekea kusimama kwa huduma za usafiri

https://p.dw.com/p/4iFue
Bavaria
Maji yakiwa yamefurika katika baadhi ya mitaa ya Jimbo la Bavaria kusini mwa UjerumaniPicha: Wolfgang M. Weber/IMAGO

Mvua kubwa zinazoendelea kunyesha Ujerumani katika maeneo mengi zimesababisha mafuriko katika maeneo mengi nchini humu.

Kwa mujibu wa msemaji wa polisi katika mji wa Kempten, kusini-magharibi mwa Munich, usiku wa kuamkia leo barabara nyingi katika eneo hilo ziligeuzwa kuwa nyeupe na mvua ya mawe huku karibu watu 320 wakiripoti kuhitaji msaada wa dharura katika eneo hilo.

Soma zaidi. Kimbunga Beryl chaipiga Jamaika na sasa kinaelekea Mexico

Maafa makubwa zaidi yameshuhudiwa katika miji ya jimbo la kusini mwa Ujerumani la Bavaria na maeneo ya mpakani na Austria ambako barabara nyingi zimefunikwa na maji, miti ikianguka na kupelekea kusimama kwa huduma za usafiri kwa muda ingawa mpaka sasa hakuna majeruhi walioripotiwa.

Mamlaka ya hali ya hewa ya Ujerumani imeripoti kuwa mvua za radi zinatarajiwa kuendelea wikiendi hii hasa katika maeneo ya Pwani.