Mafuriko yaathiri elimu magharibi na kati mwa Afrika
16 Oktoba 2024Shirika hilo la Save the Children pia limesema mafuriko nchini Nigeria, Mali, Niger na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo yamesababisha takriban watu milioni moja kuyahama makazi yao.
Katika taarifa,Save the Children imesema kuwa mvua hizo ambazo hazijawahi kushuhudiwa, zimesababisha mzozo unaozidi kuwa mbaya wa elimu baada ya kuharibiwa kwa shule, majengo ya shule kutumiwa kama makazi ya muda kwa waliopoteza makazi yao na kuhama kwa familia kutoka maeneo ya karibu na shule.
Soma pia:Watoto milioni 1.8 wamekimbia makaazi yao ukanda wa Sahel
Save the Children, imetoa wito kwa serikali kupanga haraka mikakati mbadala ya watoto wanaokosa masomo na kuhakikisha kuwa shule zinawekwa katika hali ya kustahimili zaidi hali mbaya ya hewa katika siku zijazo.
Pia iliwataka wafadhili wake kuongeza msaada kwa watu walioathirika.