Maelfu ya watu wakimbilia mji wa Homs katikati mwa Syria
6 Desemba 2024Matangazo
Hayo yanatokea wakati makundi ya waasi yakiendeleza mashambulizi yao dhidi ya vikosi vya serikali upande wa kusini.
Makundi hayo ya waasi tayari yameiteka miji muhimu ya Aleppo upande wa kaskazini na Hama katikati mwa nchi, hatua hiyo ikionekana kuwa pigo kwa Rais Bashar al-Assad, karibu miaka 14 baada ya maandamano dhidi yake kuzuka kote Syria.
Shirika hilo linalofuatilia vita vya Syria lenye makao makuu yake nchini Uingereza, limeeleza kuwa maelfu ya watu walianza kukimbia na kuelekea maeneo ya pwani ya magharibi, ngome kuu ya serikali.
Umoja wa Mataifa watoa wito wa kupunguza uhasama Syria
Mkaazi mmoja wa eneo hilo la pwani amesema maelfu ya watu wameanza kuwasili kutoka Homs kutokana na hofu ya mashambulizi ya waasi.