Maelfu wakusanyika kumuunga mkono Chamisa nchini Zimbabwe
22 Agosti 2023Matangazo
Taifa hilo la kusini mwa Afrika litafanya uchaguzi mkuu wa urais na wabungekesho Jumatano.
Mikutano mingi ya mwanasiasa huyo wa upinzani ilipigwa marufuku na baadhi ya wafuasi wake walishambuliwa na watu wanaoshukiwa kuwa wanaharakati wa chama tawala cha ZANU-PF.
Chamisa mwenye umri wa miaka 45 anawania urais dhidi ya Rais Emmerson Mnangagwa.
Kura hiyo inatizamwa kwa karibu kama kipimo cha umaarufu wa chama cha ZANU-PF.
Chama hicho kimekuwa madarakani tangu Zimbabwe ilipopata uhuru miaka 43 iliyopita.
Uchumi wa Zimbabwe umegubikwa na mfumuko mkubwa wa bei uliopanda kwa asilimia 175.8 mnamo mwezi Juni na hatimae kupungua mwezi Julai kwa asilimia 101.
Benki ya Dunia inaelezea viwango vikubwa vya madeni visivyo endelevu vinavyoikabili Zimbabwe.