1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maelfu wajiunga na maandamano ya kupinga ukatili Marekani

Sekione Kitojo
1 Juni 2020

Waandamanaji wanaopinga ubaguzi kwa mara nyingine  tena wameingia  mitaani katika miji nchini Marekani Jumapili kupaza sauti  zao za hasira dhidi ya ukatili wa polisi.

https://p.dw.com/p/3d5xv
Kanada Toronto | Proteste nach dem Tod von George Floyd in Minneapolis durch Polizeigewalt
Picha: picture-alliance/NurPhoto/A. Shivaani

Wakati  huo huo utawala wa rais Donald Trump  uliwaita wanaoongoza maandamano hayo yaliyofanyika  katika  usiku wa  siku  tano  kuwa  ni  magaidi wa ndani ya nchi. 

Wakati  viongozi  wa maeneo  mbali mbali  wakitoa  wito kwa  raia kuonesha  hasira zao kwa  njia  ya  uadilifu  kuhusiana  na  kifo cha mtu  mmoja mweusi ambaye  hakuwa  na  silaha, amri ya kutotembea usiku iliwekwa  katika  miji  kama  Los Angeles, Houston na Minneapolis , ambayo  imekuwa  kitovu  cha  machafuko.

Maandamano  yaliyokuwa  yakiangaliwa  kwa  karibu  zaidi  yalitokea nje ya ofisi  za  serikali  katika  mji pacha wa  Minneapolis  wa St.Paul ambako maelfu  kadhaa  ya  waandamanaji  walijikusanya kabla ya  kuandamana  katika  barabara  kuu.

USA Boston Proteste nach dem Tod von George Floyd | Plakate I Can't Breathe
Waandamanaji wakibeba bango lililoandikwa maneno aliyoyasema George Floyd kabla ya kufariki, kwa pamoja wanasema "hatuwezi kupumua"Picha: Imago Images/AFLO/K. Hiromi

"Tuna watoto wa kiume  weusi, tuna ndugu weusi , hatutaki wafe. Tumechoka kuona  hili likitokea, kizazi hiki hakina hilo, tumechoka kukandamizwa," alisema  Muna Abdi, mwanamke  mweusi  mwenye umri  wa  miaka 31  ambaye  alijiunga  na  maandamano.

Mamia  ya  polisi na  vikosi vya  ulinzi  wa  taifa viliwekwa  kabla  ya maandamano  licha  ya  kuwa  hakukuwa  na  ripti  za  ghasia.

Wakati  hakuna  hali  iliyojirejea  la  ghasia  za kiwango  kikubwa ambacho  kilitikisa  miji  katika  siku  za  hivi  karibuni, waporaji walivamia  maduka na  maeneo  mbali  mbali katika  mji wa Philadelphia.

Wachoma moto

Waandamanaji  walichoma  moto  karibu  na  Ikulu ya  Marekani  ya White House wakati hali  ya  wasi  wasi  na  polisi  ilipopanda wakati  wa  siku  ya  tatu  mfululizo ya  maandamano  ya  usiku yaliyofanyika  kujibu kifo cha  George Floyd mikononi mwa  polisi mjini  huko Minesota.

Saa  moja  kabla ya  kuanza kwa  amri ya kutotembea  usiku , polisi walifyatua  mabomu  kadhaa  ya  kutoa  machozi na  mabumu ya kuwatisha waandamanaji  katika  kundi  la  waandamanaji  wapatao 1,000, kwa kiasi  kikubwa  wakiwatawanya watu  kutoka  katika eneo  la  uwanja  wa  Lafayette  katika  barabara  kutoka  Ikulu  ya White House, na  kuwatawanya  waandamanaji  katika  mtaa  huo.

USA Washington vor dem Weißen Haus | Proteste nach dem Tod von George Floyd
Waandanaji wakikusanyika kuandamana karibu na Ikulu ya Marekani ya White HousePicha: Getty Images/AFP/M. Ngan

Waandamanaji  walikusanya  vibao vya alama  za  barabarani  na vizuwizi  vya  plastiki  na  kuchoma moto  katikakti ya  mtaa  H. Baadhi  walishusha  bendera  ya  marekani  kutoka  katika  jengo  la karibu  na  kuitupa  katika  moto.

Rais Trump  aliwapongeza wanajeshi wa kikosi cha  ulinzi wa taifa kwa  kusema, "pongezi kwa  walinzi  wetu  wa  taifa kwa  kazi  nzuri waliyofanya  mara  walipowasili Minneapolis , Minesota, usiku  wa jana," alisema  hayo  katika  ukurasa wa  Twitter na  kuongeza kuwa "wanapaswa kutumika  katika  majimbo  mengine kabla  ya kuchelewa !"