Uvamizi wa kijeshi la Urusi katika mji wa bandari na wenye viwanda wa Mariupol nchini Ukraine kati ya Machi na Mei mwaka 2022, ulisababisha maafa makubwa. Maelfu ya raia waliuawa, wengine walijeruhiwa na wale walionusurika waliishi kwa wiki kadhaa katika mazingira magumu wakiwa hawana huduma na vifaa vya msingi. Shambulio la kijeshi na mzingiro wa Mariupol vilichukuliwa kuwa kinyume cha sheria.