Wiki hii dunia imeadhimisha siku ya watu wenye ualbino , kuikumbusha dunia kuwatambua na kuwahusisha watu wenye ualbino katika mipango ya Maisha bila ubaguzi. Ni miaka 15 tangu lilipoibuka balaa la mauaji ya albino kwa kuwakata viungo vya miili yao, ambapo nchini Tanzania takribani watu 75 wenye Ualbino waliuwawa. Mbiu ya Mnyonge kutoka kwake Prosper Kwigize inafuatilia suala hilo.