Madaktari: Mtu wa saba huenda ´amepona´ virusi vya UKIMWI
19 Julai 2024Matangazo
Mjerumani huyo, ambaye ametaka kutotajwa majina, amepachikwa jina la "mgonjwa anayefuata wa Berlin".
Daktari mtafiti katika hospitali ya chuo kikuu cha Charite cha Berlin Christian Gaebler, amesema timu yao haiwezi kuthibitisha kwa uhakika ikiwa virusi vya VVU vimetokomezwa kabisa kwa mgonjwa huyo.
Mgonjwa wa awali wa Berlin, Timothy Ray Brown, alikuwa mtu wa kwanza kutangazwa kuponywa VVU mnamo mwaka 2008. Hata hivyo, Brown alikufa kutokana na saratani mwaka 2020. Mwanaume huyo aligunduliwa mara ya kwanza kuwa na maambukizi ya VVU mwaka 2009.
Mafanikio ya upandikizaji Seli Shina kwa watu wenye VVU, yametangazwa kabla ya kufanyika kwa mkutano wa 25 wa kimataifa wa UKIMWI katika mji wa Munich mapema wiki ijayo.