1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Macron kumpokea Biden katika ziara rasmi mjini Paris

Sylvia Mwehozi
8 Juni 2024

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron anatarajiwa hivi leo kumpokea Rais wa Marekani Joe Biden ambaye yupo katika ziara rasmi ya kitaifa nchini humo.

https://p.dw.com/p/4gocC
Frankreich Omaha Beach | Emmanuel Macron und Joe Biden
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron (kushoto) akiwa na Rais wa Marekani Joe Biden walipokutana Omaha Beach Normandy, Ufaransa wakati wa D-Day:06.06.2024Picha: Virginia Mayo/AP/picture alliance

Viongozi hao wawili wanapanga kufanya mazungumzo ya pande mbili katika makazi rasmi ya Macron, na kisha kufuatiwa na mkutano wa pamoja na waandishi wa habari.

Rais wa Marekani aliyeko ziarani nchini Ufaransa aliwasili siku ya Jumatano na kushiriki katika maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 80, tangu vikosi vya Marekani na nchi washirika vilipoanzisha operesheni ya kuikomboa ulaya dhidi ya Ujerumani iliyokuwa ikitawaliwa na Wanazi wakati wa vita vikuu vya pili vya dunia, katika kile kinachoitwa  D-Day.

Biden na Macron watajadili changamoto mbalimbali za kimataifa ikiwa ni pamoja na msaada wa Ukraine na kuandaa mkutano wa G7 huko Italia na ule wa NATO mjini Washington mwezi Julai.