1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Macron azuru makaburi ya Wayahudi yaliyoharibiwa

20 Februari 2019

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ameyatembelea makaburi ya Wayahudi baada ya makaburi 80 ya Wayahudi kuharibiwa kwa makusudi. Wanasiasa wa pande zote walaani vitendo vya chuki dhidi ya Wayahudi

https://p.dw.com/p/3DiSr
Frankreich | Demonstration gegen Antisemitismus in Paris
Picha: imago/PanoramiC/S. Caillet

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron hapo sikum ya Jumanne alikwenda kwenye jimbo la Alsace mashariki mwa Ufaransa ambapo makaburi 80 ya Wayahudi yaliharibiwa kwa makusudi na kukashifishiwa kwa kaulimbiu za kifashisti.

Macron alikutana na viongozi wa Wayahudi wa sehemu hiyo na kusisitiza dhamira ya kupambana na chuki dhidi ya Wayahudi katika kila namna itakayojitokeza.Vitendo 541 vya chuki dhidi ya Wayahudi viliripotiwa mwaka jana nchinni Ufaransa. Takwimu hizo zinawakilisha ongezeka la aslimia 74, kulinganisha na mwaka 2017.

Rais Macron amelaani uharibu  uliofanywa kwenye makaburi hayo ya Wayahudi, amesema  chuki dhidi ya Wayahudi ni kinyume na maadili ya Ufaransa na amesema katika Twitter kwamba taifa lote la Ufaransa, linapaswa kupinga kadhia hizo. 

Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amelaani vitendo hivyo vya kushtusha vilivyomfanya waziri wa mambo ya ndani wa Israel atoe wito kwa Wayahudi wa nchini Ufaransa kurejea nyumbani, Israel. Waziri Mkuu Netayahu amesema jambo lililotokea ni la kushtusha nchini Ufaransa. Makaburi 80 ya Wayahudi yameharibiwa na kubandikwa nembo za Manazi na watu wanaowachukua Wayahudi. Natoa wito . Ni balaa linalomhatarisha kila mtu na siyo sisi Wayhudi tu ni lazima chuki hiyo ilaaniwe popote inapojitokeza.

Jamii ya Waislamu nchini Ufaransa waandamana kupinga chuki dhidi ya Wayahudi
Jamii ya Waislamu nchini Ufaransa waandamana kupinga chuki dhidi ya WayahudiPicha: picture-alliance/T. Camus

Wakati huo huo waziri mkuu wa Poland alibatilisha mpango wa nchi yake wa kupeleka ujumbe kwenye mkutano wa mjini Jerusalem baada ya waziri wa mambo ya nje wa Israel, Israel Katz kusema kwamba Poland ilishirikiana na mafashisti na kuongeza kuwa Wapolish walinyonya maziwa ya kuwatia chuki dhidi  ya Wayahudi.

Balozi wa Marekani nchini Poland amemtaka waziri huyo wa Israel aombe radhi. Balozi huyo  Georgette Mosbacher amesema Israel na Poland ni washirika thabiti wa Marekani na kwamba hawapaswi  kujibizana. Balozi huyo wa Marekani nchini Poland amesema ushirika wao ni muhimu na kwamba matatizo  yote yanaweza kutatuliwa baina ya nchi hizo mbili.

Kwa mujibu wa tahtmini ya msomi Jürgen Ritte, mhadhiri kwenye chuo kikuu cha Sorbonne mjini Paris vitendo vya chuki dhidi ya Wayahudi vimeongezeka nchini Ufaransa. Msomi huyo amesema chuki hiyo  inatoka sehemu mbalimbali. Msomi huyo Ritte amesema chuki hiyo inatokana na itikadi kali za kidini na kisiasa. Pia amesema kwamba miongoni mwa wanaharakati wa vizibao vya manjano pia wapo watu  wanaowachukia Wayahudi.

Katika matukio mengine ya hivi karibuni nchini Ufaransa mwanafalsafa na mwandishi riwaya wa Kiyahudi Alain Finkielkraut alizomewa na kubughudhiwa kandoni mwa maandamano ya wanaharakati wa vizibao vya  manjano.

Mwandishi:Zainab Aziz/RTRE/APE/p.dw.com/p/3DgAA

Mhariri:Sekione Kitojo