Macron awataka washirika wa Ukraine kutokuwa ''waoga''
6 Machi 2024Macron ameongeza kuwa anabaki na msimamo wake kuhusu matamshi ya kutatanisha aliyotoa wiki iliyopita ya kutoondoa uwezekano wa kutumwa kwa wanajeshi wa mataifa ya Magharibi nchini Ukraine, yalioibua mshtuko kote barani Ulaya.
Wakati wa ziara katika Jamuhuri ya Czech yenye lengo la kushinikiza kuhusu mpango wa kununua silaha nje ya Ulaya kwa Ukraine, Macron amesema kuwa Ulaya inafikia wakati ambapo itakuwa lazima kutokuwa na uoga.
Soma pia: Marekani: Hatuna mpango wa kupeleka wanajeshi nchini Ukraine
Hata hivyo, ikulu ya White House ya Marekani imesema kuwa Ukraine haijawahi kuomba msaada wa vikosi vya Magharibi.
Msemaji wa Baraza la Usalama wa Taifa la Marekani John Kirby, amewaambia waandishi habari mjini Washington kwamba Rais Zelensky hajatuma ombi hilo na kwamba anaomba tu silaha.
Waziri wa ulinzi wa Ujerumani amesema matamshi ya Macron hayasaidii.