1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Macron kujadili wimbi la ghasia za kisiwa cha Caledonia

15 Mei 2024

Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa anafanya kikao na mawaziri waandamizi mchana huu kujadili wimbi la ghasia linaloshuhudiwa kwenye kisiwa cha bahari ya Pasifiki kilicho chini ya milki ya Ufaransa cha New Caledonia.

https://p.dw.com/p/4fs5F
Neukaledonien | Unruhe Verfassungsentwurf
Picha: Djelyna Lebonwacalie/REUTERS

Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa anafanya kikao na mawaziri waandamizi mchana huu kujadili wimbi la ghasia linaloshuhudiwa kwenye kisiwa cha bahari ya Pasifiki kilicho chini ya milki ya Ufaransa cha New Caledonia.

Kikao hicho cha dharura cha masuala ya ulinzi na usalama kwa kawaida huwaleta pamoja rais Macron na maafisa kadhaa wa ngazi ya juu wa serikali ikiwemo waziri mkuu, mawaziri wa ulinzi, uchumi, mambo ya nje na wa ya ndani.

Kimeitishwa baada ya mtu mmoja kuuwawa na makumi ya watu ikiwemo maafisa wa polisi kujeruhiwa katika machafuko yanayoendelea katika kisiwa cha New Caledonia kupinga mageuzi ya katiba yanayoshinikizwa na Ufaransa.

Mageuzi hayo ambayo ni lazima yaidhinishwa na bunge la Ufaransa yatawapatia haki ya kupiga kura watu walioishi kwenye kisiwa hicho kwa angalau miaka 10. Hata hivyo magauezi hayo yanapingwa na kundi linalopigania uhuru wa kisiwa cha Caledonia ambalo linasema yatapunguza nguvu ya jamii ya wazama katika ngazi za maamuzi.