1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Machafuko ya Ukingo wa Magharibi yazusha wasiwasi tena

8 Machi 2023

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa katika Mashariki ya Kati Tor Wennesland amezihimiza Israel na mamlaka ya Palestina kutuliza machafuko yanayoongezeka katika Ukingo wa Magharibi.

https://p.dw.com/p/4OOBh
Israel | Israelis demonstrieren in Jerusalem gegen umstrittene Justizrevisionen
Picha: Mahmoud Illean/AP/picture alliance

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa katika Mashariki ya Kati Tor Wennesland amezihimiza Israel na mamlaka ya Palestina kutuliza machafuko yanayoongezeka katika Ukingo wa Magharibi. Kauli hiyo imejiri siku moja baada ya uvamizi wa karibuni kabisa wa Israel kuwauwa watu sita. Wennesland amesema katika taarifa kuwa Baraza la Usalama limezungumza kwa kauli moja, likizitolea wito pande zinazohusika kuwa tulivu na kujizuia na vitendo na maneno ya uchochezi.Israel yatumia ndege kushambulia Gaza

Hii ni baada ya kushuhudiwa mapigano makali wakati Israel ilivamia mji wa Jenin, eneo tete la kaskazini mwa Ukingo wa Magharibi, ambapo wanajeshi waliwauwa Wapalestina sita, akiwemo mwanachama mmoja wa Hamas anayetuhumiwa kwa kuwauwa walowezi wawili wa Israel mwezi jana.