JamiiPapua New Guinea
Machafuko ya kikabila yaua watu 30 Papua New-Guinea
16 Septemba 2024Matangazo
Vikosi vya usalama nchini humo vimepewa mamlaka ya dharura kuchukuwa hatua ya kuzima machafuko hayo.
Polisi imesema machafuko hayo kwa mara ya kwanza yalizuka mwezi Agosti baada ya wachimbaji madini wasiokuwa na kibali kumjeruhi mmiliki mmoja wa ardhi katika bonde la Porgera, eneo mojawapo ambako kuna utajiri mkubwa wa dhahabu.
Mazungumzo ya kutafuta amani yalishindikana na hali imegeuka kuwa machafuko mabaya ya kikabila,ambapo jana Jumapili watu 30 waliuwawa huku mamia ya wanawake na watoto wakiachwa bila makaazi baada ya majumba kutiwa moto.
Maafisa wawili pia ni miongoni mwa waliouwawa. Kamishna wa polisi David Manning amesema nguvu itatumika kurudisha utulivu katika eneo hilo la milimani.