1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mashahidi wa Uganda warejeshwa miaka 140 baada ya kuuawa

12 Septemba 2024

Mashahidi wa Uganda warejeshwa miaka 140 baadae

https://p.dw.com/p/4kWw2
Antike Statue
Picha: IMAGO/Pond5

Mafuvu ya Waganda wawili waliouawa karibu miaka 140 iliyopita kwa kukataa kukufuru Ukristo yamerejeshwa nchini humo kutoka Roma pamoja na mabaki mengine.

Wakatoliki 22 pamoja na Waanglikana 23, wengi wao wanaume wenye umri mdogo waliuawa mwaka 1885 na 1886, kwa amri ya Mfalme wa Buganda, ambayo hivi sasa ni sehemu ya Uganda, aliekuwa na wasiwasi juu ya kuongezeka kwa ushawishi wa Ukristo.

Wakijulikana kama mashahidi wa Uganda, wote walipitia mateso, wengi wao kwa kuchomwa wakiwa hai, na wengine wakiuawa kwa kutumia mikuki au visu.

Soma pia: Papa Francis awasifu mashahidi wa Uganda

Jumuiya ya Kikatoliki ya White Fathers, maarufu kama Wamishonari wa Afrika, ilituma mabaki ya mashahidi hao wawili mjini Roma, ambako walitangazwa watakatifu, huku wengine wakibakishwa Uganda.

Chuo Kikuu cha Mashahidi nchini Uganda kimesema kupitia mtandao wa X kwamba mabaki yaliorejeshwa yanahusisha mfupa wa taya la Matia Mulumba, na mfupa usiobainishwa wa Charles Lwanga, pamoja na minyororo iliyotumiwa kuwafunga na misalaba iliyotengenezwa kutokana na miti walikofungwa.

Miaka 100 ya uhujaji wa mashahidi wa Uganda