1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JangaUganda

Mabaki ya ´mashahidi wa Uganda´ kurejeshwa Septemba

6 Mei 2024

Uganda itapokea mabaki ya watu wawili kati ya makumi ya wale wanaofahamika kama "mashahidi wa Uganda" ambao walinyongwa zaidi ya karne moja iliyopita kwa kukataa kuukana ukristo.

https://p.dw.com/p/4fWy5
Papa Francis nchini Uganda
Papa Francis alitembelea eneo la kumbukumbu ya ´mashahidi wa Uganda´ huko Namugongo.Picha: Reuters/J. Akena

Hayo yametangazwa jana Jumapili na kanisa katoliki nchini humo.

Waumini 22 wa kikatoliki na 23 wa madhehebu ya Anglikana walinyongwa kati ya mwaka 1885 na 1886 kwa amri ya aliyekuwa mfalme wa milki ya Buganda, ambayo sasa ni sehemu ya Uganda, kutokana na hofu ya kiongozi huyo juu ya ushawishi uliokuwa unaongezeka wa dini ya Kikristo.

Wote waliuawa kikatili -- wengi wao walichomwa moto wakiwa hai na wengine walidungwa visu au mikuki. Shirika la Kimishionari la White Fathers lilipeleka mabaki ya mashahidi wawili huko Roma, Italia ambako walitangazwa kuwa watakatifu.

Mifupa ya wawili hao inatarajiwa kurejeshwa Uganda mwezi Septemba na itaweka kwa ajili ya maonesho katika Chuo Kikuu cha Mashahidi wa Uganda.