Jaji Mkuu na Gavana wa Benki Kuu wajiuzulu Bangladesh
10 Agosti 2024Jaji Mkuu Obaidul Hassan alijiuzulu baada ya waandamanaji kumuonya juu ya matokeo ya kutojiondoa uongozini. Gavana wa benki kuu Abdur Rouf Talukde pia alijiuzulu lakini kujiuzulu kwake bado, hakujakubaliwa kufuatia umuhimu wa nafasi yake, hii ikiwa ni kulingana na mshauri wa masuala ya fedha katika wizara ya fedha Salehuddin Ahmed.
Awali manaibu gavana wanne walilazimishwa kujiuzulu baada maafisa 300 hadi 400 wa benki kuandamana dhidi ya kile walichosema ni ufisadi wa viongozi wao wa juu.
Yunus asifu ´ukombozi wa pili´ wa Bangladesh
Haya yanajiri wakati Kiongozi wa mpito nchini Bangladesh Muhammad Yunus akitoa wito wa kuvumiliana katika masuala ya imani za kidini, akisema wajibu wake sasa ni kuijenga Bangladesh mpya isiyokuwa na migawanyiko ya kidini.