Maandamano ya kupinga ukatili wa polisi kufanyika Ufaransa
23 Septemba 2023Maandamano ya kupinga ukatili wa polisi na ubaguzi wa rangi yamepangwa kufanyika kote nchini Ufaransa leo hii, ikiwa ni takriban miezi mitatu baada ya kifo cha mvulana mwenyse asili ya Kiarabu wakati wa ukaguzi wa polisi katika kituo kimoja karibu na mji mkuu, Paris. Waandaaji wametoa wito wa mikusanyiko katika jiji la Paris na miji mingine. Waandamanaji wanagadhibishwa na ubaguzi wa kimfumo, ongezeko la kutokuwa na usawa katika jamii, hali ambayo kimsingi inaathiri wakaazi wa vitongoji masikini, wengi wao wakiwa Wafaransa wenye asili ya Kiarabu na Kiafrika.Nahel, kijana aliyekuwa na umri wa miaka 17, aliuwawa kwa kupigwa risasi na polisi katika mkasa ambao ulizusha ghasia zilizoambatana na matukio ya uchomaji moto na uporaji, zilizodumu kwa siku kadhaa na kuathiri taifa zima.