1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maandamano ya February 13 dhidi ya wanazi

13 Februari 2012

13.02 ni siku ya kukumbuka jinsi mji wa Dresden ulivyoshambuliwa mwaka 1945.Tarehe hiyo inatumiwa na wanazi tangu mwishoni mwa miaka ya 90 kueneza propaganda zao.Wananchi walio wengi wanaipinga tathmini yao .

https://p.dw.com/p/142Pq
Bundespolizisten bereiten sich am Montag (13.02.2012) auf ihren Einsatz zu den Gedenkfeiern und Demonstrationen am Sächsischen Landtag in Dresden vor. Am 13. Februar wird hier der Opfer der Luftangriffe auf Dresden im Zweiten Weltkrieg gedacht und gleichzeitig ziehen Neonazis durch die Stadt. Foto: Oliver Killig dpa/lsn
Polisi wajiandaa kukabiliana na machafuko pindi yakizuka katika kuadhimisha siku mji wa Dresden ulipoteketezwa kwa mabomu mwaka 1945Picha: picture-alliance/dpa

Ilikuwa muda mfupi kabla ya saa nne za usiku,februari 13 mwaka 1945,pale mamia ya madege,mengi yao yakiwa ya Uingereza yalipoporomosha mabomu dhidi ya mji wa Dresden.Dakika 15 zilitosha kuweza kuiteketeza robo tatu ya mji huo.Saa chache baadae,wimbi la pili la hujuma likafuatia na kuzusha dharuba ya moto.Watu zaidi ya 20 elfu waliangukia mhanga wa janga hilo la moto.

Wanahistoria wanashindana bado mpaka leo kama kulikua na haja yoyote ya kijeshi kuuteketeza mji wa Dresden.Miezi kama mitatu baadae utawala uliokuwa ukijulikana kama "enzi ya tatu" ukasalim amri bila ya masharti.

Tangu mwaka 1946,mashambulio  ya Februari 13 dhidi ya Dresden yanakumbukwa kwa milio ya kengele makanisani.

Mit zahlreichen Aktionen protestieren Dresdner am 1.5.2002, wie hier am Schloss, gegen einen Aufmarsch von rund 800 Neonazis in ihrer Stadt. Unter dem Motto "Dresden gegen Rechts - Jetzt Gesicht zeigen" wurden die Prosteste von mehr als 180 Vereinen, Initiativen, Parteien, Gewerkschaften und Kirchen unterstützt. Über 13000 Menschen nahmen nach DGB-Angaben teil.
Maandamano dhidi ya wanazi mambo leoPicha: picture-alliance/dpa

Lakini tangu mwaka 1998 kumbu kumbu hizo zimeingia dowa.Makundi ya siasa kali za mrengo wa kulia yanaitumia tarehe hiyo kwa kukanusha madhambi ya Ujerumani katika vita na pia mauwaji ya halaiki ya wayahudi-Holocaust.Maandamano ambayo mwanzo yalikuwa yakiwateremsha njia wanazi mambo leo wasiozidi mia moja,hivi sasa yanahudhuriwa na watu wasiopungua 6500.Yanaitishwa kila siku ya Februari 13 kwa kile wanachokiita " Maandamano ya msiba."

Ili kuonyesha msimamo wao dhidi ya wafuasi wa siasa kali za mrengo wa kulia,wakaazi wa Dresden na wengineo kutoka maeneo mbali mbali ya Ujerumani wanaandaa pia maandamano yao.Mwaka jana walikuwa watu zaidi ya 15 elfu waliokamatana mikono mfano wa mnyonyoro kulaani  msimamo wa wanazi mambo leo.

Maandamano kama hayo yanatarajiwa pia kuanyika hii leo mjini Dresden.

Blick auf die Dresdner Altstadt am Samstag (15.08.2009) waehrend des Dresdner Stadtfests.Foto: Sebastian Kahnert
Picha ya mji wa Dresden na kanisa la "Frauenkirche"Picha: picture alliance/ZB

Mmojawapo wa waandalizi wa maandamano hayo,mwanasiasa wa chama cha walinzi wa mazingira mwenye asili ya kituruki,Memet Kilic anasema:"Maandamano ya amani yanaweza kutoa sura ya vizuwizi.Ikiwa maelfu ya watu wataandamana dhidi ya wanazi mambo leo,basi wanazi hawatapata tena uwanja wa kuweza kuandamana.Ndio maana anasema anawatolea mwito watu waandamane kwa amani."

Mwito huo ameutoa kufuatia machafuko yaliyozuka mwaka jana pale polisi walipojaribu kuwatawanya waandamanaji waliozingira njia kinyume na sheria.

Mwandishi:Marcel,Fürstenau/   Hamidou Oummilkheir

Mhariri:Abdul-Rahman,Mohammed