Maafisa wawili wakuu wa FIFA wakamatwa
3 Desemba 2015Picha za video zinaonyesha polisi wakifika katika hoteli hiyo ya Baur au Lac mjini Zurich na kisha kuondoka wakiwa na watu wawili.
FIFA imesema itashirikiana kikamilifu na wachunguzi kuhusiana na tukio hilo. Wizara ya sheria ya Uswisi imesema katika taarifa kuwa wanaume hao wawili ambao hawajatambuliwa kwa majina, wanatuhumiwa kwa kupokea mabilioni ya dola kama hongo. Hongo hiyo inahusishwa na haki za mauzo za michuano ya kufuzu dimba la Kombe la Mataifa ya Amerika Kusini – Copa America na Kombe la Dunia
Hii ni mara ya pili kwa hoteli hiyo inayotumiwa na maafisa wa FIFA kuvamiwa na polisi mwaka huu huku tuhuma za rushwa zikiendelea kulisakama shirikisho hilo la kandanda ulimwenguni.
Mkutano wa siku mbili wa kamati kuu ya FIFA unaendelea mjini humo. “Fifa itaendelea kushirikiana kikamilifu na wachunguzi wa Marekani kama inavyokubalika katika sheria ya Uswizi, pamoja na uchunguzi unaoendeshwa na afisi ya mwanasheria mkuu wa Uswisi.
Mwandishi: Bruce Amani/AP
Mhariri: Yusuf Saumu