1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSaudi Arabia

Maafisa wakuu wa Magharibi na Kiarabu kukutana Saudi Arabia

27 Aprili 2024

Maafisa wakuu wa nchi za Magharibi na Kiarabu wanatarajiwa kukutana wiki ijayo mjini Riyadh, Saudi Arabia kujadili vita vilivyodumu kwa miezi kadhaa katika Ukanda wa Gaza

https://p.dw.com/p/4fG2a
Majengo yalioharbiwa na shambulizi la Israel katika Ukanda wa Gaza katika mapigano yanayoendelea kati ya Israel na kundi la wanamgambo la Hamas mnamo Aprili 25.04.2024
Majengo yalioharbiwa na shambulizi la Israel katika Ukanda wa GazaPicha: Abed Rahim Khatib/dpa/picture alliance

Vyanzo hivyo vimearifu kuwa mawaziri wa mambo ya nje wa Saudi Arabia, Misri, Qatar, Umoja wa Falme za Kiarabu na Jordan, watakutana siku ya Jumatatu mjini Riyadh pamoja na wenzao wa Ujerumani, Uingereza, Ufaransa na Italia.

Maafisa wa mataifa ya Kiarabu pamoja na mwakilishi wa Palestina wakutana

Vyanzo hivyo vimeliarifu shirika la habari la dpa kwa sharti la kutotambulishwa kwamba maafisa hao wa mataifa ya Kiarabu ikiwa ni pamoja na mwakilishi wa Mamlaka ya Palestina, watakutana leo ili kujadili msimamo wao wa pamoja kabla ya mkutano huo wa Jumatatu.

Soma pia:Saudia yakosoa shambulio la Israel kambi ya wakimbizi Gaza

Hata hivyo vyanzo hivyo vimeeleza kuwa afisa huyo wa Palestina hatahudhuria mazungumzo hayo na wajumbe wa Magharibi. Saudi Arabia inaanda kongamano la kimataifa la uchumi kuanzia kesho Jumapili hadi Jumatatu.