SiasaSudan
Maafisa wa UN waonya kuongezeka kwa mateso ya raia wa Sudan
3 Novemba 2023Matangazo
Mamadou Dian Balde, afisa mkuu wa kikanda wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi (UNHCR) amesema ni mateso ya kutisha kuona miezi sita ya mzozo Sudan, na tayari watu 6,000,000 wamelazimishwa kuyahama makazi yao, ikiwa ni wastani wa milioni moja kwa mwezi.
Mnamo Alhamisi, afisa mwingine wa Umoja wa Mataifa katika eneo hilo, Dominique Hyde, alisema ameshuhudia "hali ya kutisha" kwenye mpaka na Sudan ambapo karibu watu 10,000 waliokimbia vurugu wamewasili katika siku tatu zilizopita.
Tangu mwezi Aprili mwaka huu, mzozo kati ya jeshi na kundi la RSF nchini Sudan tayari umesababisha pia vifo vya watu 9,000.