Ujumbe wa Marekani wakutana na wawakilishi wa Taliban, Doha
1 Agosti 2023Taarifa ya Wizara ya Mambo ya Kigeni ya Marekani imesema ujumbe wa Marekani katika mazungumzo hayo yaliyofanyika katika mji mkuu wa Qatar Jumapili, ulielezea wasiwasi mkubwa kuhusiana na mzozo wa kiutu na haja ya kuendelea kuyaunga mkono mashirika ya misaada na taasisi za Umoja wa Mataifa zinazotoa msaada kwa kuzingatia kanuni za kibinaadamu nchini Afghanstan.
Ujumbe wa Marekani waelezea wasiwasi kuhusu unyanyasaji
Aidha walionyesha wasiwasi mkubwa kuhusu matukio ya kukamatwa watu, ukandamizaji wa vyombo vya habari, na mipaka kuhusu masuala ya kidini.
Waliohudhiuria ni pamoja na Mwakilishi Maalum wa Marekani Thomas West na Mjumbe Maalum anayehusika na Wanawake wa Afghanistan, Wasichana na Haki za Binaadamu Rina Amiri, pamoja na Karen Decker, mkuu wa ujumbe wa Marekani nchini Afghanistan. Taarifa hiyo haikutoa maelezo ya wawakilishi wa Taliban walioshiriki mazungumzo hayo