1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu 19 wameuawa kwenye mashambulizi ya Israel huko Gaza

4 Januari 2025

Waokoaji katika Ukanda wa Gaza wamesema karibu watu 19, wakiwemo watoto wanane, wameuawa katika mashambulizi ya Israel. Jeshi la Israel halijazungumzia mashambulizi hayo.

https://p.dw.com/p/4oopz
Mashambulizi ya Israel kwenye Ukanda wa Gaza
Maafisa Gaza wasema watu 19 wameuawa kwenye mashambulizi ya IsraelPicha: Rizek Abdeljawad/Xinhua/dpa/picture alliance

Shirika la Ulinzi wa Raia limesema shambulizi la anga mapema Jumamosi, liliilenga nyumba ya familia ya al-Ghoul katika Mji wa Gaza na kuwauwa watu 11, saba kati yao wakiwa ni watoto. Msemaji wa shirika hilo Mahmud Bassal amesema nyumba hiyo ya ghorofa mbili, iliyokuwa imewahifadhi watu kadhaa waliopoteza makazi yao, iliharibiwa kabisa.

Jeshi la Israel halijazungumzia mashambulizi hayo. Kwingineko, shirika la ulinzi wa raia limesema maafisa watano wa usalama, waliopewa jukumu la kuongozana na misafara ya msaada, waliuawa kwenye shambulizi la Israel wakati wakisafiri kwenye gari katika mji wa kusini wa Khan Yunis. Jeshi la Israel halijajibu tuhuma hizo.