1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maafisa 100 wa polisi ya DRC wakimbilia Uganda

5 Agosti 2024

Msemaji wa jeshi la Uganda amesema maafisa 100 wa polisi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wamekimbiliaUganda mwishoni mwa juma huku mapigano kati ya waasi wa M23 na jeshi la Kongo yakipamba moto.

https://p.dw.com/p/4j8Ef
Wanajeshi wa Uganda wakilinda mpaka wa nchi hiyo na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Wanajeshi wa Uganda wakilinda mpaka wa nchi hiyo na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.Picha: Glody Murhabazi/AFP/Getty Images

Meja Kiconco Tabaro alisema siku wa Jumatatu (Agosti 5) kwamba maafisa hao wa polisi waliingia Uganda kupitia mpaka wa Ishasha katika wilaya ya Kanungu kusini magharibi mwa taifa hilo la Afrika Mashariki. 

Tabaro alieleza kuwa polisi hao wa Kongo waliokuwa na bunduki 43 na risasi kadhaa walipokonywa silaha hizo.

Soma zaidi: DRC imekua rasmi mwanachama wa saba wa EAC

Msemaji huyo wa jeshi la Uganda aliongeza kuwa wanawake waja wazito, akina mama wanaonyonyesha na watoto wadogo walikuwa miongoni mwa wakimbizi hao kutoka Kongo.

Katika muda wa siku nne zilizopita, zaidi ya wakimbizi 2,500 wamekimbia vita nchini Kongo na kuingia nchini Uganda.