1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maadhimisho ya siku ya wazee ya kimataifa

Manasseh Rukungu1 Oktoba 2004

Taasisi maalum ya umoja wa mataifa imetangaza ripoti mpya kuhusu hali ya maisha ya raia wanaoingia katika umri wa uzeeni duniani ambao unaonyesha kwamba idadi ya watu wazima inazidi kupanda hasa katika nchi zilizo tajiri. Utafiti muhimu kwa huduma za maisha ya kijamii duniani.

https://p.dw.com/p/CHiO
Hermann Dörnemann, mzee mwenye umri mkubwa kabisa hapa Ujerumanj, miaka 110.
Hermann Dörnemann, mzee mwenye umri mkubwa kabisa hapa Ujerumanj, miaka 110.Picha: dpa

Miaka 35 iliyopita ulianzishwa utaratibu maalum kwenye umoja wa mataifa wa kuchunguza namna ujamii zinavyozidi kuwa na watu wengi wazima na matatizo yatokanayo na hali hiyo kwa vizazi vijavyo. Mwanzoni mwa mwaka 1980 umoja wa mataifa uliunda taasisi maalum kwa kushirikiana na serikali ya Malta, ambayo jukumu lake lilikuwa ni kuchunguza matatizo ya kijamii, kiuchumi na kisiasa ambayo huzushwa na jamii kuzidi kuwa na wazee wengi na hatua gani zinazofaa katika kuyatatua matatizo hayo.

Majuma machache yaliyopita mwenzetu kijana aliandika ripoti kuhusu siku ya vijana ya kimataifa na kushikilia kwamba, kwa kweli si maisha rahisi mtu kuwa ni kijana. Hayo ni kweli kabisa, lakini inabidi kuongeza kwamba, mtu mzima kuzidi kuwa ni mzee haya pia si maisha rahisi hasa kwa wale ambao wamekuwa wakifanya kazi gumu katika maisha yao. Hapa haijaliwi jinsi maisha ya vijana yalivyo na sura mbali mbali na ya kutotendewa kwa haki, kulinganisha na maisha ya raia wanaoingia katika umri wa uzeeni, hasa kuanzia umri wa miaka 60 na ambao wamekuwa tangu utotoni wakifanya kazi gumu. Hii ni hali ya maisha ambayo haiwezi kueleweka rahisi na vijana, hasa kwa sababu hawawezi kukadiria namna wazee kuanzia umri huo wa miaka 60 walivyokuwa wakiishi tangu utotoni.

Uchunguzi wa taasisi hii ya umoja wa mataifa, ni mkakati muafaka na wa kutegemewa iwapo yanatakiwa kutabiriwa maendeleo ya wakati ujao katika jamii duniani. Uchunguzi huo unatuelimisha namna ya kuwaelekeza njia wataalamu wa maisha ya kijamii pamoja na wale wanaojifanya ni watetezi wa dunia bora ambapo binadamu anaendesha maisha huru. Sababu ni kwa kuwa utafiti na maendeleo ya binadamu, hushawishi sana hali ya maisha ya kiraia kupita maamuzi ya kisiasa.

Mtu mwenye shauku ya kujua mambo ya kisiasa, kwa kweli hupatwa na kigugumizi, anapotupia jisho tarakimu. Utangazaji wa tarakimu huonekana kama ni mchango katika maisha ya binadam, kwanza tarakimu humshtusha na kumfanya mtu kutafakari na hatimaye humfanya kuingiwa na hali ya wasiwasi. Kwani licha ya pengo lililopo kati ya matajiri na maskini duniani pia liko pengo lingine ambalo ni la hatari katika shuguli za kisiasa: Nalo ni kuzidi kwa idadi ya wazee katika maeneo yaliyo tajiri duniani, ambayo inaifanya kuwa gumu jitihada ya kuhakikisha huduma za kijamii.

Leo hii thuluthi moja ya raia waliokwishatimiza umri wa miaka 60 duniani, ambao wanakisiwa ni zaidi ya Milioni 235 inakutikana katika nchi tajiri, na baada ya miaka 4o ijayo idadi yao itavuka Milioni 400. Na mtu akitupia jicho wazee waliokwishatimiza umri wa miaka 8o, hapana shaka anaifahamu bora hali hii, kwa sababu idadi yao itapanda na kuvuka Milioni moja katika kipindi hicho. Tarakimu hizi ni muhimu kwani zinatufafanulia hali ilivyo kwa kweli katika jamii ya mgongano wa kijamii kati ya wazee na vijana, ambao haujapatiwa utatuzi wa kisiasa.

Kuzidi kuzeeka kunawabebesha matatizo ya kijamii kwa pamoja watu wazima na vijana. Na jamii hizi mbili zinashindwa au mara nyingi hazina ushujaa wa kutafuta mikakati inayofaa ya kisiasa ya kusaidia kutatua mgongano huo katika nchi zenye kufuata misingi ya demokrasia. Ndio maana kilicho muhimu kabisa ni kufahamiwa maana ya demokrasia na uchumi wa masoko, iwapo wazee kwa vijana wanataka kuendesha maisha salama na ya neema.