Ripoti zinasema mapigano yameendelea katika mji wa Sake ulioko kilomita 20 kutoka Goma huko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kati ya waasi wa M23 na jeshi la Kongo linalosaidiwa na vijana Wazalendo. Duru zinasema waasi wanazidi kuusogelea mji wa Goma ambao sasa unazidi kuzingirwa.