1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LUXEMBOURG:Pendekezo la Malta juu ya wahamiaji lakataliwa Ulaya

13 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBsA

Mawaziri wa mambo ya ndani kutoka nchi za umoja wa Ulaya wameshindwa kufikia suluhisho juu ya kukisaidia kisiwa cha Malta katika kukabiliana na wimbi la wahamiaji kutoka nchi za Afrika.

Katika mkutano uliofanyika huko Luxembourg,waziri wa mambo ya ndani wa Ujerumani Wolfgang Schäuble alisema umoja huo wenye wanachama 27 kimsingi uko tayari kugawana majukumu lakini hawakuweza kuafikiana.

Pendekezo la visiwa vya Malta la kutaka watu wanaotaka kuwa wahamiaji Ulaya kugawanywa katika nchi hizo halikuungwa mkono na wengi.

Wakosoaji wanahofia wimbi la wakimbizi litaongezeka zaidi ikiwa pendekezo hilo litakubaliwa.

Mkutano huo wa Luxembourg umefanyika kufuatia visiwa hivyo vya Malta kukataa kuwapokea watu 27 waliokuwa wakijaribu kuingia katika visiwa hivyo.