Luxembourg: Waziri mkuu wa Luxembourg Jean Claude Juncker anahisi duru mpya ya majadiliano
15 Desemba 2003Matangazo
kuhusu katiba ya Ulaya haitafanyika kabla ya nusu ya pili ya mwaka ujao.Akihojiwa na gazeti la "Financial Times Deutschland" waziri mkuu wa Luxembourg amesema anaamini mazungumzo yataanza upya Uholanzi itakapokabidhiwa zamu ya mwenyekiti wa umoja wa Ulaya.Ameonya dhidi ya mpango ulioshauriwa na waasisi wa Umoja wa Ulaya:Ujerumani,Ufaransa,Italy na nchi tatu za Benelux,yaani Ubeligiji,Uholanzi na Luxembourg wa kushirikiana zaidi hadi katiba mpya itakapopitishwa.Duru ya kwanza ya mazungumzo ya nchi hizo sita huenda ikaitishwa mwezi january au february mwakani.