Luxembourg kunafanyika uchaguzi wa bunge
8 Oktoba 2023Tangu mwaka 2013 taifa hilo linatawaliwa na muungano wa vyama vitatu unaoongozwa na Waziri Mkuu wa kiliberali, Xavier Bettel.Kwa zingatio la kura ya maoni ya hivi karibuni, muungano wake na wenye kuhusisha vyama vya Greens and Social Democrats ambao kwa sasa unashikilia viti 31 kati ya 60 bungeni, unaweza kupata kura za kutosha kudumisha wingi wake kwa muhula mwingine madarakani.Hata hivyo, chama cha upinzani cha Christian Social People's Party, ambacho kimeingia kwenye kinyang'anyiro hicho na mgombea wake mkuu Luc Frieden kimetajwa kuongoza katika kura za maoni.Kupiga kura ni lazima katika taifa hilo la pili kwa udogo katika Umoja wa Ulaya likiwa na jumla ya watu 660,000 huku wengine 88,000 wanaoishi nje ya taifa hilo wakiwa na msamaha wa kutoshiriki zoezi hilo.