SiasaBelarus
Lukashenko atoa wito wa mazungumzo kati ya Urusi na Ukraine
25 Aprili 2024Matangazo
Rais Lukashenko amesema masuala yaliyojadiliwa kati ya Urusi na maafisa wa Ukraine nchini Uturuki katika wiki za mwanzo za vita kati ya mataifa hayo mawili, yanaweza kutumika kama mahali pa kuanzia mazungumzo hayo.
TASS pia imemnukuu Lukashenko, mshirika wa karibu wa Rais wa Urusi Vladimir Putin,akisema kwamba kunaweza kuwa na ''maangamizi ya dunia'' ikiwa Urusi itatumia silaha za nyuklia kulipiza kisasi kwa vitendo vya mataifa ya Magharibi.
Mara kwa mara, Urusi imekuwa ikionya kwamba uungaji mkono wa mataifa ya Magharibi kwa Ukraine kunayaweka katika mapambano ya moja kwa moja na Urusi na huenda ukachochea mzozo wa nyuklia.