1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Lukashenko asema hatawazuia wahamiaji kuingia Umoja wa Ulaya

19 Agosti 2024

Rais wa Belarus, Alexander Lukashenko amesema taifa lake halina mpango wa kuwazuwia wahamiaji kupitia nchini mwake kuelekea katika mataifa ya Umoja wa Ulaya.

https://p.dw.com/p/4jdyz
Rais wa Belarus Lukashenko
Alexander Lukashenko, rais wa BelarusPicha: Alexey Belkin/Russian Look/NEWS.ru/picture alliance

Lukashenko amesema hawezi kuwekewa vikwazo na umoja huo na wakati huo huo ategemewe kuwazuia wahamiaji wasiingie kwenye ukanda huo.

Kiongozi huyo wa Belarus ameyasema hayo leo Jumatatu alipofanya mahojiano na televisheni moja ya Urusi.

Mamlaka za Umoja wa Ulaya, hasa Poland zimekuwa zikiwatuhumu Rais wa Urusi Vladimir Putin na Lukashenko ambaye ni mshirika wake wa karibu, kwa kuwapitisha kwa makusudi wahamiaji kuingia kwenye mataifa wanachama wa Umoja wa Ulaya tangu mwaka 2021 na kuwapatia visa pamoja na pasi za kusafiria.