1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LUANDA : Familia za watu 2,000 zatishiwa na janga la njaa

16 Septemba 2005
https://p.dw.com/p/CEaY

Takriban familia za watu 2,000 katika majimbo matano ya Angola zinakabiliwa na baa la njaa huku utapia mlo ukiaathiri hadi asilimia 60 ya idadi ya watu wake.

Katika uchunguzi wa shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula katika baadhi ya maeneo yalioko mbali Waangola wanaishi kwa kutegemea mlo mmoja kwa siku wakati watoto wenye umri wa miaka sita hadi miezi 20 wanateseka sana kutokana na utapia mlo kwa vile maji ya kunywa hayapatikani.

Uchunguzi huo ulifanywa kwenye majimbo ya Huambo, Kwanza-sul,Bie,Huila na Benguela kati kusini mwa Angola ambapo watu milioni moja na laki saba wanaishi kutathmnini ya mahitaji ya kibinaadamu.