London yatarajia Meya wa kwanza Muislamu
6 Mei 2016Shughuli ya kuhesabu kura za kumtafuta meya wa mji wa London Uingereza ikiwa inaendelea, kuna matarajio kwamba mji huwo kwa mara ya kwanza utapata Meya wa Kiisilamu katika uchaguzi wenye ushindani mkali.
Sadiq Khan (45), mbunge wa chama cha Labour, anaonesha kuwa na wafuasi wengi na anaweza kuchukua nafasi ya Meya wa sasa wa chama tawala cha Conservative, Boris Johnson.
Ushindi wa Khan kama Meya wa London utakiinua juu kidogo chama cha Labour, ambacho kimepoteza wafuasi wengi katika jimbo la Scotland licha ya kuwa hapo kabla kiliwahi kuwa na uungwaji mkono mkubwa.
Chama cha SNP chashinda Scotland
Chama kinachounga mkono kujitenga kwa Scotland cha SNP kimeshinda wingi wa viti kwa mara ya tatu mfululizo katika uchaguzi wa bunge wa Scotland, kwa mujibu wa matokeo ya mwisho yaliyotolewa leo hii.
"Hakuna shaka chama cha SNP kimeshinda kwa mara ya tatu mfululizo katika uchaguzi wa bunge la Scotland. Hilo halijawahi kufanyika kabla katika historia ya bunge la Scotland. Usiku wa leo tumeandikisha historia," amesema Nicola Sturgeon, kiongozi wa chama cha Scotland National Party (SNP).
Hata hivyo, chama hicho kinahitaji viti viwili zaidi ili kuweza kuongoza serikali nchini humo. Kimeshinda viti 63 kati ya 129, ambavyo havitoshi kuunda serikali kikiwa peke yake, na hivyo kunahitajika kuundwa serikali ya pamoja na chama kidogo kama vile chama cha kijani.
Matokeo hayo yaanshiria chama cha SNP nacho pia kimepoteza uugwaji mkono, ikilinganishwa na matokea ya uchaguzi uliopita ambapo kilijinyaulia viti 69 na kuweza kuongoza serikali.
Aidha chama cha kizalendo cha Scotland kimeibuka mshindi wapili kikiwa kimeshinda viti 31, huku chama cha Labour kikishika nafasi ya tatu kwa kushinda viti 24.
Waingereza walipiga kura siku ya Alhamisi kuchagua wabunge katika jimbo la Scotland pamoja na Wales, huku London ikiwa inachaguwa Meya mpya.
Ikiwa zimebaki wiki chache kabla ya Uingereza kuitisha kura ya maoni itakayoamuwa iwapo itabaki ama itajitoa katika Umojaw aUlaya, uchaguzi huwo unaangaliwa na wengi kama kipimo cha uugwaji mkono wa viongozi wa vyama vikuu.
Nguvu ya kiongozi wa chama kikuu cha upinzani cha labour Jeremy Corbyn inatazamwa kwa uangalifu zaidi, ikiwa hii ni mara yake ya kwanza chama hicho kinapigiwa huku kikiongozwa naye.
Mwandishi: Yusra Buwayhid/afp/rtre/ap
Mhariri: Yusuf Saumu