London. Waziri mkuu wa Uingereza anapanga kufanya mkutano wa kimataifa kuhusiana na Uislamu wa imani kali.
21 Julai 2005Waziri mkuu wa Uingereza Tony Blair anapanga kufanya mkutano wa kimataifa kuhusu makundi yenye imani kali katika dini ya Kiislamu kufuatia mashambulio ya mabomu dhidi ya mji wa London.
Kiongozi huyo wa Uingereza amesema kuwa juhudi za kimataifa zinahitajika kupambana na ugaidi kutoka katika mizizi yake, ambayo amesema iko ndani zaidi na imesambaa.
Bwana Blair amesema kuwa kiasi cha nchi 26 zimeathirika na mashambulizi yanayohusishwa na kundi la al Qaeda tangu mwaka 1993.
Baada ya mashambulizi ya hapo Julai 7, Blair pia amesisitiza uaminifu wake kwa majeshi ya ulinzi nchini humo kufuatia taarifa kuwa Uingereza ilishusha tathmini yake ya kitisho kutokana na ripoti ya siri ya kijasusi kiasi cha wiki tatu kabla ya mashambulizi hayo.