1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON : Marekani yashutumiwa kwa ukiukaji wa haki za binaadamu

26 Mei 2005
https://p.dw.com/p/CFA6

Shirika la kimataifa la kutetea haki za binaadamu la Amnesty International limetowa repoti kali juu ya hali ya haki za binaadamu duniani kote.

Repoti hiyo inazishutumu serikali nyingi kwa kutelekeza ahadi zao za kulinda haki za binaadamu kwa mwaka 2004.Katika repoti hiyo ya kila mwaka ya kurasa 300 shirika hilo la haki za binaadamu limesema serikali ya Marekani imeharibu hali ya haki za binaadamu kutokana na msimamo wake wa kutesa na ushughulikiaji wa wafungwa.

Mjini Berlin Barbara Lochbihler wa shirika la Amnesty tawi la Ujerumani amewaambia waandishi wa habari kwamba nchi nyingi zimekuwa zikifuata mfano huo wa Marekani.Mjini Washington msemaji wa Ikulu ya Marekani Scott McCellan ameita repoti hiyo kuwa mzaha.Shirika hilo la kimataifa la kutetea haki za binaadamu pia limeishutumu jumuiya ya kimataifa kwa jumla kwa kushindwa kuchukuwa hatua kukomesha mgororo wa kibinaadamu kama ule uliopo Dafur magharibi mwa Sudan.