1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Lissu aahidi mabadiliko makubwa CHADEMA

22 Januari 2025

Kiongozi mpya wa Chama cha CHADEMA, Tundu Lissu amesema ananuwia kufanya mabadiliko makubwa ndani ya chama hicho ikiwemo kuweka ukomo wa mihula ya uongozi wa nafasi ya mwenyekiti ambao utaanza na yeye.

https://p.dw.com/p/4pU7U
Tanzania Tundu Lissu
Mwenyekiti mpya wa Chadema Tundu LissuPicha: Emmanuel Herman/REUTERS

Lissu alichaguliwa Jumanne usiku kuwa mwenyekiti CHADEMA akimshinda Freeman Mbowe ambaye alikuwa kiongozi wa chama hicho kwa miongo miwili.

Ameanza kazi, kwa kutangaza kuwa anakwenda kumchagua Katibu Mkuu  na manaibu katibu wakuu wa chama hicho katika mkutano wa baraza hilo Jumatano usiku. 

Mbowe ampongeza Lissu kwa ushindi Chadema

Pia ametangaza nia ya kuifanyia mabadiliko katiba ya chama hicho na kuweka ukomo wa Madaraka kwa viongozi wa juu wa chama.

Soma pia: Freeman Mbowe akubali kushindwa uenyekiti CHADEMA

Lisu ameahidi kubadili mfumo wa viti maalum vya udiwani na ubunge kwa wanawake ndani ya chama hicho ili kuwepo na ufanisi katika nafasi hizo.

Matokeo ya uchaguzi huu yameibua hisia tofauti miongoni mwa wanasiasa na wachambuzi wa kada za siasa wakisema uchaguzi huu umetoa funzo.