Pazia la Ligi Kuu Tanzania Bara msimu mpya wa 2022/2023 limefunguliwa kwa mechi kati ya Ihefu na Ruvu Shooting huku timu ya Namungo ikiwa na miadi na Mtibwa Sugar. Yanga bingwa wa Ngao ya Jamii. Gumzo linaendelea mtaani kufuatia Derby ya Kariakoo iliyopigwa mwishoni mwa juma kati ya Wekundu wa Msimbazi Simba na Yanga. Naomi William (pichani) anaripoti kutoka Dar es Salaam.