1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Libya yafunga kisima cha mafuta wakati mzozo ukitokota

Sylvia Mwehozi
19 Aprili 2022

Viongozi wa kikabila kusini mwa Libya wamekifunga kisima kikubwa zaidi cha mafuta nchini humo. Ni hatua ya karibuni kabisa ya kufungwa kisima cha mafuta wakati kukiwa na mzozo mkali kati ya serikali mbili pinzani.

https://p.dw.com/p/4A6If
Libyen | Öl- und Gas Bohrinsel im Mittelmeer
Picha: Antonio Sempere/Europa Press/abaca/picture alliance

Viongozi wa kikabila kusini mwa Libya wamekifunga kisima kikubwa zaidi cha mafuta nchini humo. Ni hatua ya karibuni kabisa ya kufungwa kisima cha mafuta wakati kukiwa na mzozo mkali kati ya serikali mbili pinzani. Uzalishaji mafuta katika kisima cha Sharara umesitishwa na shirika la kiserikali la National Oil Corp. limetangaza amri ya Force Majeure, ambayo ni mbinu ya kisheria inayoiwezesha kampuni kuondokana na majukumu yake ya kimkataba kwa sababu ya mazingira yasiyo ya kawaida. Shirika hilo mafuta limeiita hatua ya kufungwa kisima hicho kuwa ya kipuuzi na inayoonesha mkwamo unaoendelea nchini humo. Viongozi wa kikabila katika mji wa jangwani wa Ubari, walisema walikifunga kisima hicho kulalamikia serikali ya Waziri Mkuu anayekabiliwa na mbinyo Abdul Hamid Dbeibah. Kisima cha Sharara kinazalisha karibu mapipa 450,000 kwa siku.