Miaka 10 tangu aliyekuwa rais wa Libya Muammar Gaddafi kupinduliwa madarakani na kuuawa, Libya bado haijafufuka kutokana na mapinduzi hayo. Marekani, Ufaransa na Uingereza zilitoa msaada wa kijeshi katika mapinduzi hayo. Bruce Amani amezungumza na Ali Mali mchambuzi wa siasa za Afrika kutoka kisiwa cha Mayote na kwanza amemuuliza tathmini yake ya Libya miaka kumi baada ya kifo cha Gaddafi.