1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Liberia kuangalia madai ya rushwa kabla ya uchaguzi tena

2 Novemba 2017

Mahakama Kuu ya Liberia imesema itafanyia uchunguzi madai ya kwamba pamekuwa na rushwa kabla ya uchaguzi wa duru ya pili wa rais uliopangwa kufanyika wiki ijayo. Wagombea ni George Weah na Joseph Boakai.

https://p.dw.com/p/2muBU
Vizepräsident Joseph Nyuma in Monrovia Liberia
Picha: Reuters/T. Gouegnon

Mahakama kuu ya Liberia imesema itaangalia kuhusu madai ya rushwa kabla ya uchaguzi wa duru ya pili wa rais uliopangwa  kufanyika wiki ijayo kati ya mchezaji wa zamani wa kandanda George Weah na makamu wa rais Joseph Boakai, kama wagombea wanaowania kuchukua nafasi ya rais wa kwanza mwanamke, mshindi wa nishani ya amani ya Nobel Ellen Johnson Sirleaf.

Mgombea aliyeshika nafasi ya tatu Charles Brumdkine na chama chake cha Leberty wanadai kulikuwa na mapungufu katika  uchaguzi wa duru ya kwanza mwezi Oktoba, na amedai kurudiwa kwa uchaguzi. Waangalizi wa uchaguzi kutoka Umoja wa Ulaya, hata hivyo, wamesema hawajaona matatizo makubwa. 

Kwa mujibu wa matokeo ya duru ya kwanza, Weah alipata asilimia 38 ikilinganishwa na asilimia 29 za Boakai.