1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Leverkusen waufungua msimu wa Bundesliga kwa ushindi

24 Agosti 2024

Mabingwa Bayer Leverkusen waliendeleza walikoachia na kuanza msimu mpya wa Bundesliga kwa ushindi wa dakika za mwisho wa mabao 3 - 2 ugenini dhidi ya Borussia Moenchengladbach Ijumaa usiku.

https://p.dw.com/p/4js3n
Ujerumani | Borussia Moenchengladbach vs. Bayer 04 Leverkusen | Bundesliga 0:2
Leverkusen walianza kutetea taji lao la Bundesliga kwa ushindi wa 3 - 2 dhidi ya Borussia MoenchengladbachPicha: Joerg Niebergall/Eibner-Pressefoto/picture alliance

Msimu uliopita, Leverkusen ilishangaza kwa namna ilivyofunga mabao kadhaa ya dakika za lala salama na muhimu katika safari yao ya kushinda taji lao la kwanza la ligi kuu na kuumaliza msimu bila kupoteza mechi hata moja.

Soma pia: Bayer Leverkusen yabeba Kombe la Super Cup la Ujerumani

Na inaonekana muujiza huo wa dakika za majeruhi umerudi kwa msimu wa 2024-25. Mabingwa hao watetezi walikuwa kifua mbele 2 - 0 kabla ya Gladbach chini ya kocha Gerardo Seoane kupambana na kurejesha mabao hayo lakini Leverkusen ikapewa penalti katika dakika ya 10 ya muda wa nyongeza.

Katika mechi za Jumamosi, Stuttgart ambao walimaliza wa pili msimu uliopita watacheza dhidi ya Freiburg, RB Leipzig watakuwa nyumbani dhidi ya Bochum na Borussia Dortmund watawakaribisha Eintracht Frankfurt dimbani Signal Iduna Park. Jumapili, Bayern Munich wataanza msimu wao dhidi ya Wolfsburg.