1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Leverkusen vinara wapya wa Bundesliga

14 Desemba 2020

Kinyang'anyiro cha Bundesliga kimechukua muelekeo mwingine baada ya kukamilika mechi za duru ya 11. Schalke na Leverkusen zilionesha namna timu mbili zinavyoweza kuwa katika viwango tofauti katika ligi yenye timu 18 tu.

https://p.dw.com/p/3mhzg
Fußball Bundesliga Bayer 04 Leverkusen - TSG Hoffenheim
Picha: Thilo Schmuelgen/AFP/Getty Images

Ni mapema mno lakini Bayer Leverkusen wamekamata usukani wa ligi baada ya ushindi wa 3 – 1 dhidi ya Hoffenheim. Katika upande wa mkia, Schalke walipoteza uongozi wa 2 – 1 na kulazimishwa sare ya 2 -2 dhidi ya Augsburg. Klabu hiyo sasa imecheza mechi 27 bila ushindi.

Iliwachukua mabingwa watetezi Bayern Munich dakika 66 kusawazisha dhidi ya Union Berlin na kuponyoka ugenini na pointi moja baada ya sare ya 1 – 1. Hiyo ina maana kuwa wanatoshana pointi na RB Leipzig waliowarraua Werder Bremen 2 – 0. Wote wana 24, moja nyuma ya vinara Leverkusen

Lakini tukio kubwa lilitokea dimbani Signal Iduna Park, ambapo wenyeji Borussia Dortmund waliduwazwa na Stuttgart, kwa kubamizwa 5 – 1. Favre alisema haya baada ya mechi hiyo

kichapo hicho kilikuwa ni msumari wa mwisho katika jeneza la Favre…maana saa 24 baadaye, klabu ikampiga kalamu. Kocha mpya wa Dortmund Edin Terzic ataanza kazi yake rasmi wakati timu yake itaposafiri kesho kupambana na Werder Bremen, huku miamba hao wa Bundesliga wanaokabiliwa na mgogoro wakilenga kupata ushindi wao wa kwanza katika mechi nne. Bayern watacheza dhidi ya Wolfsburg Jumatano, Leverkusen watakuwana na mahasimu wao wa mtaani Cologne wakati Leipzig ikipambana na Hoffenheim.

AFP/reuters/DPA/AP